Simulizi ya kweli..SARAFINA SEASON 3(Historia ya GAIDI KENNY!)
Msimuliaji.................Kenny Jonas
Mwandishi................Jack Mambo
Whstp........................0744872552
Call.............................0716352102
Umri...........................18+
GROUPS ZINAPOTEA LAKINI PAGE ZINAISHI... LIKE PAGE YANGU ILI USIKOSE HADITHI ZANGU KILA SIKU IITWAPO LEO KARIBUNI...👉👉👉Story za Mambo
Sehemu ya 4🖤
Mapenzi yaliweka kidonda kwa Mara ya kwanza katika maisha yangu,kidonda ambacho sikujua kitapona lini?
Sikutaka kuongea kitu,nilitaka waendelee kujua kuwa niko hospitali sababu ya mwanamke niliyempenda,nimepigwa sana sababu yake!
Japo nilikuwa na maumivu makali lakini nilimhurumia sana Vivian,hasa nilipokumbuka maneno ya Idrisa alijigamba kuwa Vivian kamfuata mwenyewe na wala hana upendo nae,na akasema nimuache amtumie Kisha atamrudisha
kwangu!
Yalikuwa maneno makali Sana ambayo kwa hakika Kama angeyasikia Vivian basi angetembea kwa magoti na kuja kunitaka radhi!
Niliruhusiwa kutoka hospitali baada ya siku mbili japo ilinichukua wiki nzima kuuguza majeraha yangu ndipo nikarejea tena shuleni!
Ilikuwa ngumu kusoma dasara moja na Vivian,kila nilipomuangalia nilijikuta tu roho inauma mno!
Ajabu Vivian wala hakujali,hata nilipokutanisha naye macho alinibetulia mdomo juu kwa dharau!
Sikujua Kama Fahyma anaelewa kuwa Shoga yake anamzunguka,na wala sikuona kama yananihusu,waliendelea na urafiki wao na mimi nikajitahidi Sana kufanya mambo yangu!
Niliamua kusoma na kujiweka mbali na mapenzi kabisa,Vivian alikuwa amenipa maumivu makali mno!
Ili kumuepuka nikawa natoka naenda kusomea darasa la pili ambalo halikuwa langu ili tu nisiwe namuona Vivian!
Niliamua kuzoea ile hali na kujikuta naanza kusahau yaliyotokea!
Sikuwa na shida na Idrisa,sababu hata nikisema niwe na bifu naye nitaumia tu!
Idrisa ni kiongozi wa kundi la kihalifu jijini Mwanza!
Ana vijana ambao wamejiunga na kuanzisha genge lao la kufanya fujo tu,kwahiyo ilikuwa ili uwe kijana ambaye huwezi kuonewa ni lazima uwe kwenye makundi yao!
Niliamua kushika hamsini zangu na kufuata maisha yangu,japo iliniuma kuona nimepokonywa mwanamke niliyempenda Sana!
Wanasema hakuna siri inayodumu milele,basi ndivyo ilivyokuwa!
Mapenzi ya Vivian na Idrisa aliyagundua Fahyma,hapo ndipo urafiki na ushoga wao ukafikia tamati!
Siku hiyo nilikuwa zangu darasani nikashangaa kumuona Fahyma anamfuata Vivian na kuanza kumsema!
"Hivi wewe Vivie ni wa kutembea na mpenzi wangu kweli,Yani kumbe umemuacha Kenny ili uje unizunguke tushee penzi!"
"Aaah!shoga siku hizi mjini ujanja kushea,Cha peke yako kaburi tu ulikuwa hujui ndo nakujuza ivyo",alisema Vivian kwa nyodo na kiburi!
"Yani kwa ushoga wetu siamini kama ungeweza kunifanyia hivi!"
"Kwani tatizo nini shogaangu,mi kanipa nimekula nimeiacha,sijaondoka nayo,au amekuambia nimeichukua natembea nayo,nitolee nyege hapa umekosa bwana nini?"
"We Vivian unanijibu mimi ivyo?"
"Ulitakaje!"
Fahyma alipandisha hasira akamrukia Vivian zikaanza kupigwa,binafsi nilikuwa pembeni tu nacheka kimoyomoyo!
Hakuna mtu anapenda kumuona x wake anapata raha,niliteseka sana kwaajili yake na Mimi angalau siku ile nikamuona anateseka kidogo!
Walishikana na kuanza kuvutana nywele,mwisho akaingia bwana yao Idrisa!
"Nyie vipi?",aliuliza kwa ghadhabu!
"Wanakugombania handsome boy!",alijibu mdada mmoja mapepe mapepe!
"Oya nyie acheni upuuzi wenu,msiniharibie CV sasa sikieni siwataki wote,na kuanzia leo sitaki mazoea!"
Idrisa alikuwa kijana anayejiona sana,pesa zake za kuuza bangi na kete zilimfanya ajione tajiri shule nzima!
Vivian na Fahyma walipigwa na butwaa,waliomgombania alitamka hawataki mbele ya darasa,aibu iliyoje?
Kwa kujifaragua Vivian alimsogelea Idrisa akiamini yeye ndiyo anapendwa kuliko Fahyma,alichokutana nacho ndicho kilikuwa Cha aibu zaidi!
Alifika akataka kumkumbatia Idrisa akamkwepa akapokea kofi zito la shavu akaja kuangukia kwenye meza yangu!
"Sitaki mazoea mademu wenyewe wabaya,msyuuuu!",alisema Idrisa akafyonza kwa dharau na kuondoka zake!
Vivie alikuwa kwenye dawati langu na Kama siyo kumdaka basi angeanguka chini kabisa!
Nikimuangalia tukakutanisha macho basi akayakwepesha macho yake na kuangalia pembeni!
"Pole Vivie!"
"Msyuuuu!",alinifyonza akaondoka nikajua tu anajikosha ila anaona aibu hatari!
Hicho ndicho alichokipata baada ya kunisaliti,nilimshukuru sana Mungu kwa kunilipia kisasi,nikaamini ule usemi wa malipo ni hapahapa duniani!
Ziipita siku kadhaa huku nikiwa na mambo yangu,kipindi hicho tulikuwa tumekaribia kumaliza mtihani wa kidato cha nne!
Siku moja nikiwa zangu darasani napitia pitia masomo yangu,nilirushiwa ujumbe ambao ulinihitaji nifike kwenye Ile sehemu ambayo tulikuwa tukifanya mapenzi na Vivian enzi mapenzi yako motomoto!
Nilishtuka sana nikajiuliza Ina maana Vivian amenikumbuka?niligeuza shingo nikamuangalia Vivian ambaye wala hakuwa akiniangalia!
Nilihisi ni yeye tu,basi nikajiandaa muda wa kutoka shule nikasema ngoja nikamsikilize Vivian anataka kusema Nini?
Sifi
chi kusema kweli bado nilikuwa nampenda sana Vivie,nilitamani kusikia ananiambia turudiane,hilo ndilo lilikuwa wazo langu!
Nilifika kwenye Ile sehemu nikakaa kumsubiri Vivian,mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda mbio sana,licha ya yote aliyonifanyia bado nilihisi nataka kumsamehe!
Nilishtuka mno kumuona aliyetokea,hakuwa Vivian Kama nilivyowaza!
Nilipatwa na mshangao nikajiuliza amefuata nini pale!
Cha ajabu yeye aliponiona alitabasamu akazipiga hatua zake akinisogelea!
JE NI NANI AMEMUITA PALE KENNY?TABIRI NA USHINDE VIPANDE VITATU LEO!
UNAWEZA KUPATA HADITHI HII HADI MWISHO KWA SH 5000/= TU
Lipia hapa 👉👉👉0716352102 AU 0744872552 (NAMBA ZOTE ZIPO WHATSAPP!
#LIKE #LIKE #LIKE
#COMMENT #COMMENT #COMMENT
#SHARE #SHARE #SHARE
#MTAG_RAFIKI_YAKO_MFURAHIE_UTAMU_WA_HADITHI_PAMOJA