Simulizi ya kweli......SARAFINA SEASON 3 (Historia ya GAIDI KENNY)
Msimuliaji.................Kenny Jonas
Mwandishi................Jack Mambo
Whstp..0752761388/0744872552
Call............................0716352102
Umri...........................18+
GROUPS ZINAPOTEA LAKINI PAGE ZINAISHI... LIKE PAGE YANGU ILI USIKOSE HADITHI ZANGU KILA SIKU IITWAPO LEO KARIBUNI...👉👉👉Story za Mambo
Sehemu ya 3🖤
Nilipigwa na butwaa!sikuamini Kama yule ni mpenzi wangu Vivian,mwanamke ninayempenda kuliko maelezo!
Vivian na Idrisa walikuwa wameshikana viuno hawana habari,niliita kwa mshangao!
"Vivian!",kilichofuata hapo ulikuwa mlio wa chupa nilizokuwa nimebeba,niliziachia zikadondoka chini!
Vivian Wala hakuwa na mashaka,alinipita vile vile akiwa amekumbatiwa!
Macho yake mazuri nayoyasifia siku zote siku ile yalinionyesha dharau kubwa,aliniangalia kwa dharau huku akikatisha pembeni yangu bila wasiwasi!
"Nimeenjoi sana hakika uko vizuri Vivian!",ilikuwa ni sauti ya Idrisa!
"Hahahahhah!",alijichekesha Vivian!
Niliona haiwezekani,nionyeshwe dharau namna Ile,na hata Idrisa alijua fika kuwa Yule ni mpenzi wangu!
Nilinyoosha mkono nikamshika mkono Vivian ambaye alitaka kuutoa lakini hakuweza!
"Niachieee!wewe niniiii?",alisema Vivian lakini sikumuachia!
"We dogo vipi?",alisema Idrisa kwa sauti ya kibabe lakini sikumuhofia Wala nini,nilibadilika ghafla na kuvaa roho ya simba,sikuwahi kujiskia vile!
"We Kenny nini bwana niachie!"
" Huondoki hapa!",sijui nilipatwa wapi ujasiri ule,nilikuwa mbogo ghafla mapenzi yanauma mno!
"We dogo unaleta ubabe siyo,hunijui au siyo?"
"Idrisa kaa mbali hii kesi haikuhusu,najua unajua huyu ni mpenzi wangu!Umemfanya hainihusu!"
"We uliona wapi mapenzi yanalazimishwa!",alisema Idrisa!
"Hapo sasa!",alikazia Vivian muda huo mkono wake bado nimeung'ang'ania!
Baada ya kuona simuachii Vivian,Idrisa alinisogelea akanishika ili autoe mkono wa Vivian lakini hakufua dafu!
Baada ya hawezi kunitoa mkono si akarusha ngumi ikanipata kifuani,hapo akawa amenipandisha mori,nilirudisha shingo yangu kwa nyuma na kukirusha kichwa changu kwa kasi kikatua kwenye pua ya Idrisa nikamsikia anasema!
"Mamaaaaaa!",akashika pua yake alipoachia ni damu tu zilikuwa zinamwa
gika!
Hapo ndipo Vivian akaona nipo serious,akaanza kupiga kelele,punde tu wakaja wahudumu wakatuachanisha nikamuachia Vivian akaondoka na Idrisa huku Idrisa akiniangushia maneno makali!
"We boya umechokoza vita,utajuta mi ndiyo Idrisa umeingia Cha kike!"
Alinipa vitisho kisha wakatokomea zao,nikabaki na huzuni kuu!
Niliingia kwenye kile chumba ambacho kwa hakika nimepoteza tu pesa,maana hata niliyelipia niwe naye katoka kufanya mapenzi na mwanaume mwingine na nimeona kwa macho yangu!
Niliumia mno siku ile,nikaona dunia yote umenitenga,nilimpenda mno Vivian na Wala sikudhani Kama Kuna siku anaweza kunifanyia ushenzi!
Nilijilaza pale kitandani nikiwaza mengi,pesa yangu iliniuma mno!
Alitaka gesti nikalipa lakini ndiyo ivyo kila nilichofanya kilikuwa ni bure tu!
Mwisho nilikubali kuwa nimepoteza basi nikatoka zangu kinyonge na nikalipia na chupa niliyopasua nikawa nimebaki na shilingi elfu tatu tu!
Niliondoka kurejea nyumbani,kumbe Idrisa alikuwa ameanzisha vita kweli!
Sikujua kuwa kile kichwa kingemfanya kwenda kunikusanyia genge lake la wahuni!
Nilikatiza kwenye chochoro moja katika mitaa ya Pasiansi,nikashangaa nimezungukwa na wahuni Kama ishirini!
Nikiwa najiuliza nikamuona Idrisa akitokea katikati yao huku akiwa ameshika mkanda wa suruali!
"We fala si ulijiona Van dame,sasa nataka unionyeshe umwamba wako hapa,Mimi ndiye legend hapa kudadeki!"
Nilishtuka mno nikaangalia pa kupenyeza lakini sikuona,nilikuwa nimewekwa Kati na genge la wahuni!
Idrisa alinisogelea huku akitamba,aliponifikia alinitwanga ngumi nzito ya tumbo nikapiga goti chini kwa maumivu!
Akarusha teke na kunipiga nikaanguka chini,Kama haitoshi akaanza kunikanyaga Kama anaua nyoka!
Kibaya zaidi hakuchagua pa kukanyaga,nililia lakini hakuna aliyenisaidia,vijana wale waliogopeka jijini Mwanza na tabia zao mbovu mbovu!
"Amka tupigane basiiiii,we si unajifanya komando,amka basi!",alitamba Idrisa!
"Oya mgusenii nimemaliza!",aliwaambia na wenzake walipige!
Nilipigwa sana siku Ile,nilipigwa kila Kona ya mwili wangu,nilipigwa mpaka nikajiuliza kosa langu ni kumpenda Vivian au ni nini?
"Sasa sikia we boya,usiniletee ujinga demu wako kanipenda mwenyewe sijamuita,kwahiyo tulia nimtumie nikimchoka atakurudia,halafu nikuambie kitu,demu wako mtamu sana analia vizuri kweli,unajua alikuwa analiaje?"
'Oooh!babe nipeee we ndo unanipatia,bakora yako tamuuuu!"
"Hahahahhaha!"
Idrisa aliongea Yale maneno Kisha wenzake wakanicheka,alinipa maneno ya kashfa Kisha wakaanza tena kunipiga mpaka nikapoteza fahamu!
Hayo ndiyo mapenzi,na hapo ndipo Vivian aliponifikisha!
Mwanaume aliyemvulia nguo na kumpa penzi alikuwa anatamba na kuonyesha kuwa Vivian si chochote kabisa kwake!
Ilionyesha kuwa ni Vivian alijipendekeza kwake na Wala Idrisa hampendi!
Maneno yake yaliniumiza mno nikatamani ningekuwa na kitu nirekodi maneno Yale na kumpa Vivian wangu arudi kwangu!
Kipigo kizito kilinifanya nipoteze fahamu na sikujua kilichoendelea tena!
Nilikuja kushtuka nikiwa hospitali ya Sekou toure nimechomekewa dripu na pembeni yangu alikuwepo Mama yangu pamoja na ndugu zangu wengine walioguswa!
" Mama!"
"Mwanangu!umeamka baba"
"Niko wapi mama?"
"Uko hospitali mwanangu,pole naskia ulivamiwa na vibaka!"
Alisema mama bai nikakumbuka tu yaliyotokea na kujikuta namwanga machozi mengi mno!
"Mama nitamuua Idrisa nitamuaaa!"
"Maneno yanaumba mwanangu usiseme ivyo!"
JE NINI KITAENDELEA?VIVIAN NA IDRISA WATAFIKA WAPI?
UNAWEZA KUPATA HADITHI HII HADI MWISHO KWA SH 5000/= TU
Lipia hapa 👉👉👉0716352102 AU 0744872552 (NAMBA ZOTE ZIPO WHATSAPP!
#LIKE #LIKE #LIKE
#COMMENT #COMMENT #COMMENT
#SHARE #SHARE #SHARE
#MTAG_RAFIKI_YAKO_MFURAHIE_UTAMU_WA_HADITHI_PAMOJA