SIRI YA BAFU(13)



 Chombezo……………….SIRI YA BAFU!

Mtunzi……………………..Jack Mambo

Call…………………………..0716352102

Whtsp__0752761388/0744872552

UMRI______________18+


KUMBUKA GROUP ZINAPOTEA ILA PAGE ZINAISHI,ILI USIKOSE UHONDO WA HADITHI ZANGU INGIA HAPA LIKE PAGE YANGU,HAPO UTAKUWA NA UHAKIKA WA KUSOMA STORY ZANGU KILA SIKU ----👉👉👉  Story za Mambo 


SEHEMU YA 13

Kuna visa vinatokea vinavyosababisha mahusiano au ndoa kufikia tamati,unafika kipindi ambacho mmoja au wote wanahisi kwamba hawawezi kuendelea tena!

Sababu zipo nyingi sana,kwa wazungu Kuna sababu za kijinga tu,unaweza kusikia wanasema tumeachana kwa sababu mwenzangu yuko bize hanipi muda na kadhalika!

Lakini sababu za kiafrika Mara nyingi huwa ni fumanizi,Mara nyingi huwa ni sababu za aibu aibu tu!Sababu ambazo hata ukiulizwa na wazazi wako huwezi kusema,utaanzaje kusema nimeachwa sababu nimechepuka na mwanaume au mwanamke mwingine?

Hiyo Hali ndiyo ilimkuta Mama Jeni,alipowaza jinsi atakavyoaibika kwa kuachwa kisa ametembea na Hamza ambaye kiumri kamzidi mbali mno,alipowaza hayo alijikuta anaishiwa nguvu na kukubali kuingia kwenye mtego wa Sheila!

Alijiandaa na moja kwa moja akaingia kwa Sheila,akamkuta Sheila bado anakula chipsi zake na kwenye sofa amekaa kaka yake anachezea simu yake kubwa ya gharama aina ya iPhone toleo jipya!

"Karibu karibu Mama Jeni!",Kaka Yake Sheila alimpokea kwa tabasamu!

"Aah!Toto hilooo,wifi langu la ukwehe!",alichombeza Sheila!

Mama Jeni wala hakutia neno alikaa kwenye kitanda maana humo ndani Kuna sofa moja tu!

"Aya Aziz kazi kwako mi nilishamaliza!ngoja niwapishe!"

Alisema Sheila muda huo anataka kutoka awaache Mama Jeni na Aziz ndani,kitu ambacho Mama Jeni hakukubaliana nacho kabisa!

"Hapana Sheila usiondoke,Kama Kuna maongezi ya siri siyo hapa,naomba twende na Kaka yako sehemu salama,hapa ukitoka na kila mtu kaona ninaingia humu itakuwa ni shida!"

Wazo la Mama Jeni lilikuwa na mashiko ndiyo maana wote wakakaa kimya!

"Kwahiyo wewe unataka twende wapi?"

"Sehemu yoyote lakini siyo mtaa huu!Mimi ni mke wa mtu mnatakiwa muheshimu hilo,na ni wazi unataka kunionja tu wewe!"

"Aaah!siyo ivyo mi ikiwezekena hata akuache nikuoe mie!"

"Mmmh!pagumu hapo!"

"Ooh!oooh!nimepata wazo unaonaje mkienda mtaa wa tatu,pale wanapaita Mambo Guest House!",alisema Sheila!

"Mimi sikujui!",alisema Aziz!

"Huyu anakujua,Mama Jeni wewe tangulia sababu hatuwezi kuongozana,halafu Mimi ntakuja na broo!"

"Mmh!Aya sawa!"

Wazo la Sheila likawa limepitishwa,kwake ni Kama alikuwa na mawazo mengi Sana!

Alijua uhusiano wa Mama Jeni na Kaka yake utamnufaisha na vingi.

Alijua Kaka Yake akimpata Mama Jeni ni wazi atamoinga mizinga ya shukrani,na pia akiwaunganisha wawili hao atafanya figisu ili Hamza ajue,lengo likiwa ni kulifaidi penzi la Hamza peke yake!


Mama Jeni alitoka kishingo upande,muda huo alijua mumewe bado sana kurudi,ndiyo maana akafunga mlango na kuondoka zake!

Aliikata mitaa mpaka mtaa wa tatu,huko akakutana na bango kubwa lililosomeka,'MAMBO GUEST HOUSE'.

Alisimama akaliangalia like bango,akawaza mara ya mwisho kuingia nyumba za wageni ilikuwa kitambo Sana,kipindi hicho ndiyo mumewe alikuwa anamuhangaikia ili amuweke ndani!

Alisikitika tu akazama ndani ya Ile gesti akalipia chumba na kuingia ndani akimsubiri Kaka Yake Sheila aje ampe anachokitaka ili awe huru!


*****


Hamza siku hiyo alikuwa na tabasamu pana,maana hata njaa ilimkalia mbali siku ile!

Chapati na supu aliyokunywa lilimpa jeuri kubwa!

Alishuka akaanza kuikatiza mitaa,huku akiwa anapiga zake miluzi tu!

Kichwani alikuwa anawaza tu jinsi alivyocheza mechi za kibabe usiku akajikuta anacheka na kuongea mwenyewe kama chizi!


Ghafla alimuona mtu ambaye alihisi amemfananisha!

Alimuangalia vizuri akagundua ni Mama Jeni,hakuwa na shaka sababu alihisi pengine Mama Jeni anazungukia mikopo yake ya Madera!

Lakini alivyomuangalia vizuri aligundua Mama Jeni ni kama ana hofu fulani hivi,wakati anamtafakari mama Jeni aliangaza kulia na kushoto bahati nzuri hakumuona Kisha akazama ndani ya gesti!

"Ayaaaaaaah!huyu mama kumbe ndiyo mchafu hivi?",alijiuliza Hamza!

Kitendo Cha Mama Jeni kuingia gesti,kilimfanya aone kabisa kuwa ni mwanamke ambaye hajatulia kabisa!

Aliganda pale akiwa haamini alichokiona,alijihisi wivu Kama vile ni yeye amemuoa,akatamani kwenda kuingia gesti akaone yuko na nani?

Lakini wakati anawaza hayo kuna gari ilipaki maeneo ya Ile gesti kisha wakashuka watu wawili,mwanaume na mwanamke!

"Mungu wangu!Yule si Sheila yule jamani!"

Alijiuliza Hamza,alimuona Sheila akiwa ameongozana na mwanaume wanaingia gesti,hakuna alichowaza zaidi ya kuwa Yule ni mwanaume wa Sheila!

"Kweli kuwa uyaone,nini hiki jamani?yaani wanawake wangu wote wanaingia gesti moja,au wanajuana mmhh!

Hamza alienda mbali na kuwaza kuwa huenda hata mchezo wa Jana,walipanga wote Mama Jeni na Sheila,wakafanya naye mapenzi!

Basi kinyonge kijana Hamza akaenda zake nyumbani huku akiwa na wivu Kama wote!

Alitamani kwenda kufanya fujo lakini akajiuliza anaenda kufanya fujo kama nani?Mume wa Sheila,au mchumba wa Mama Jeni?

Alipoona Hana nafasi yoyote Kati ya hizo,akazipiga hatua zake taratibu na kushika njia ya kwenda nyumbani!

Furaha yake ilitoweka kabisa,alifika nyumbani akatua begi lake akalala,bado hakuwa na hamu ya kula!

"Kaka!Kaka!",mdogo wake alimuamsha kutoka usingizini!

"Unaitwa na Dada Sheila!"

"Dada Sheila!",alijiuliza Kuna nini?sababu kamuona Sheila ameingia gesti na mwanaume!

JE NINI KITAENDELEA?SHEILA KARUDI JE HAMZA ATAENDA?


#FULL_____SH_3500/=

#KIPANDE_SH_100/=

Lipia hapa 0716352102 (Tigopesa) au 0744872552 (mpesa)...jina Khadija matengula Kisha njoo whatsap 0752761388

#USISAHAU_KULIKE

#USIACHE_KUKOMENTI

#SHARE_KWA_WINGI

#Mtag_rafiki_yako_anayependa_hadithi_ushindeeeeeee🔥🔥🔥

Previous Post Next Post