HISTORIA YA GAIDI KENNY(06)



Simulizi ya kweli..........SARAFINA SEASON 3(Historia ya GAIDI KENNY!)

Msimuliaji.................Kenny Jonas

Mwandishi................Jack Mambo

Whstp..0752761388/0744872552

Call............................0716352102

Umri...........................18+


GROUPS ZINAPOTEA LAKINI PAGE ZINAISHI... LIKE PAGE YANGU ILI USIKOSE HADITHI ZANGU KILA SIKU IITWAPO LEO KARIBUNI...👉👉👉Story za Mambo 

Sehemu ya 6🖤

Ilikuwa ni sinema ya kutisha kuwahi kuiona katika maisha yangu,nilishuhudia Fahyma akibakwa mbele yangu!

Idrisa na kikundi chake walikuwa wamedhamiria kufanya ubaya siku ile,nahisi ulikuwa ni wivu wa mapenzi!

Huwa inatokea hasa pale ambapo mtu anamuacha mtu ilihali bado anampenda,anabaki kuumia moyoni.Kinachotokea Sasa mi kuwa atataka kumuona mwenzie anateseka,Sasa ukiwa na furaha tu na unenepe hapo ndipo mwenzio anapatwa na mhaho!

Idrisa alikuwa na wivu mkali kwa Fahyma,sio Siri kuwa ndiye mwanamke aliyempenda achana na Vivian ambaye aliingilia mapenzi yao,japo na Idrisa naye aliingilia mapenzi yangu!

Fahyma aliingiliwa na vijana Kama wanne na hapo kuna vijana kumi na mbili wanasubiri kwenye foleni!

Nilimhurumia nikatamani kufanya kitu lakini ningeanzia wapi?kamba zilinizunguka mwilini na kunibana kwenye mti nikabaki sina hata msaada wowote!

Japo hata kama ningekuwa sijafungwa kamba bado nisingeweza kupambana na wale vijana wenye silaha,Mimi siyo Rambo wala Jet li!

"Idrisaaaaa naenda kushtakiiiiiiii,naenda kushtakiiiiiiii!Aaah unaniumizaaaaa mamaaaaaaa!"

Ilikuwa ni sauti ya Fahyma akijaribu kujitetea lakini ndiyo kwanza alikuwa anaingiliwa na kijana wa tano huku kwenye foleni walibaki kumi na moja!

Niliumia sana kuona mwanamke anateseka namna Ile,nafsi yangu ilishindwa kuhimili kuona vitendo vile!

Niligeuza shingo nikamuangalia Idrisa ambaye alikuwa pembeni anavuta bangi na mkono wa kushoto kashika chupa kubwa ya konyagi anakunywa taratibu!

Kelele za Fahyma zilikuwa ni kama muziki mzuri unaoyaburudisha maskio yake na kumfanya ajiskie burudani mno!

Sikuwa na jinsi niliamua kufanya maamuzi ambayo kwa hakika nilijua yatanigharimu!

Bahati mbaya ilikuwa kwao,hawakuwa wamenifunga mdomo wangu,nilikusanya nguvu zote na kuziamishia kwenye sauti kisha nikapiga kelele kwa sauti kubwa Sana!

"Jamaniiiiiiiiiiiii!mtusaidieeeeeeeeeeeeee!"

Hapo ndipo Idrisa akakurupuka na kunifuata nilipokuwa pamoja na vijana kadhaa wakaanza kunipiga bila huruma!

"Nyie vipi?mpeni dozi huyo kahaba huyu niachieni Mimi!",aliamrisha Idrisa basi wenzake wakamtii!

Kwa wembamba wake huwezi amini Kama ndiyo kiongozi wa wale vijana na wanamtiii,sura yake nzuri ya upole haikuendana na matendo aliyokuwa akiyafanya kabisa!

"We fala unajifanya mjanja siyo!",alisema na kunipiga teke kwenye kengele zangu nikapiga yowe la maumivu,kabla hata sijatulia nikapigwa ngumi ya shavu nikatema tamu!

Muda huo napigwa bado Fahyma alikuwa akifanyiwa unyama na wale vijana!

"Ni hukuuu,sauti imetokea hukuu!"

Ilikuwa 


ni sauti ya watu waliosikia sauti yangu wakaamua kuja kuangalia Kuna nini ikibidi watoe msaada!

Sauti Ile ndiyo iliwafanya Idrisa na wenzake wasitishe walichokuwa wanafanya!

"Oyaaah!oyaaah!tusepeniiiiii!",ilikuwa sauti ya Idrisa akiwaambia wenzake,lakini muda huo huo pia watu walikuwa wameshafika tayari!

"Waleee,waleeeee!",zilikuwa ni sauti za wananchi ambao walikuwa Kama kumi na tano na mikononi wameshika silaha zao za jadi!

Idrisa na wenzake walikurupuka na kuanza kukimbia huku na huko kila mtu alipita njia Yake!

Wananchi walifanikiwa kuwakamata vijana watatu na kuwapa kipigo Cha maana Kisha wakawekwa chini ya ulinzi!

Nilikuwa nalia tu muda wote,kwa maumivu ya kipigo na kitendo nilichokishuhudia!

Walinifungulia nikawahi kumfuata Fahyma nikakuta kafumba macho Yale katulia,haraka nikachukua nguo zake na kumsitiri!

Nilisikiliza mapigo ya moyo wake nikagundua yanadunda japo kwa mbali Sana!

"Jamaniiii tumbebeniii,tumbebeniiiii tumuwahishe hospitali!",nilipaza sauti ndipo watu wakaja tukambeba na kushuka naye chini maana si mnajua tena vilima vya Mwanza!

Tulishuka mpaka tukapata usafiri wa bodaboda,nikakaa na Fahyma Kisha tukapelekwa kituoni kwanza kupata PF3!

Tuliandika maelezo haraka,basi Fahyma akapelekwa hospital na kuanza kupatiwa matibabu!

Mimi pia nilipewa matibabu nikapumzishwa kidogo kutokana na kilichotokea!

Taarifa zilifika nyumbani haraka mama yangu akaja na majirani kadhaa!

Vivyo ivyo kwa wazazi wa Fahyma ambao walikuwa ni watu wenye uwezo kifedha!

Wazazi wangu walifika na kunijulia hali,lakini katika Hali ya kushangaza nilishangaa maaskari wameingia kwenye wodi na kunipiga pingu kisha wakaninyanyua nikiwa bado na bandeji zangu!

"Uko chini ya ulinzi!"

"Nimefanyaje?Mimi..Mimi..jamani nilitekwa nilikuwa na...!"

"Kijana acha kelele,uko chini ya ulinzi na chochote utakachoongea saivi kitachukuliwa kama ushahidi!"

"Jamani...Mimi...sihusiki mamaaaa mamaaaa waambie basiii mi sihusiki!"

"Jamani kwani mwanangu si mnaona hajakosea kitu jamani,si mnaona hata yeye kaumizwa!"

Mama alijaribu kuingilia lakini akaishia kusukumwa na kuangukia kichwa akapoteza fahamu palepale!

"MAMAAAAAAAAA!"

Nilipiga kelele lakini muda huo nilikuwa nimepigwa tanganyika jeki nikatolewa na kwenda kutupiwa kwenye difenda!

JE NINI KITAENDELEA ?KIJANA KENNY ATAFANYA NINI?


UNAWEZA KUPATA HADITHI HII HADI MWISHO KWA SH 5000/= TU

Lipia hapa ðŸ‘‰ðŸ‘‰ðŸ‘‰0716352102 AU 0744872552 (NAMBA ZOTE ZIPO WHATSAPP!


#LIKE #LIKE #LIKE

#COMMENT #COMMENT #COMMENT

#SHARE #SHARE #SHARE

#MTAG_RAFIKI_YAKO_MFURAHIE_UTAMU_WA_HADITHI_PAMOJA 

Previous Post Next Post