Jack Mambo:
Simulizi ya kweli.......SARAFINA SEASON3 (Historia ya GAIDI KENNY)
Msimuliaji.................Kenny Jonas
Mwandishi................Jack Mambo
Whstp..0752761388/0744872552
Call............................0716352102
Umri...........................18+
GROUPS ZINAPOTEA LAKINI PAGE ZINAISHI... LIKE PAGE YANGU ILI USIKOSE HADITHI ZANGU KILA SIKU IITWAPO LEO KARIBUNI...👉👉👉Story za Mambo
Sehemu ya 1🖤
Naitwa Kenny,wengi wananiona kama mwanaume katili nisiyefaa,wananiona kama nawachukia wanawake sana,ndiyo ngoja nikuambie kitu,nawachukia mno hasa hawa wenye kipato!
Na mjue siku zote chuki huja kwa sababu,ni mara chache sana mtu kumchukia mtu bila sababu,hizo ndizo tunaita chuki binafsi!
Je unataka nikuambie kwanini nawachukia wanawake,kwanini nimeishi nikiwatesa na nisikubali kuona wana furahia maisha yao?
Basi usijali fuatana na mimi nikupe mkasa wa maisha yangu,uone milima na mabonde niliyopitia hadi kufikia kuwa Kenny huyu ambaye unamuona kama gaidi!
Karibu Sana,tega sikio lako kwa makini,wenye kupika mpike kabisa ndiyo msome story yangu,maana mtaunguza na kunipa lawama!Wenye kuoga waoge kabisa na wenye kula wale pia,halafu baada ya hapo chukua juisi baridi tandika jamvi lako unisikilize!
***
Siyo kwamba sikuwahi kuwa malaika katika maisha yangu,la hasha!Niliwahi kuwa na utu,Niliwahi kuwa binadamu Kama wengine!
Ni binadamu hawa ndiyo wanawageuza binadamu wenzao kuwa wanyama,hata Osama ni binadamu aliyewahi kuwa malaika lakini Marekani hao hao ndiyo waliyombadilisha na kuamua kuwa gaidi akatikisa dunia!
Bahati mbaya sana sitasimulia story ya Osama leo,niko hapa kuandika story ya maisha yangu!
Ilikuwa asubuhi moja tulivu sana,mama yangu alikuja kunigongea ili niende shule,siku zote alinihusia kuwa nisome sana,alisema kuwa ni elimu pekee itatuokoa kutoka kwenye maisha tuliyokuwa tunaishi!
Nilikuwa nikifanya ivyo,nikisoma kwa bidii sana tu,na matokeo darasani hayakuwa mabaya!
Lakini mambo yalibadilika nikiwa kidato cha nne,ni hapo nilikutana na msichana mrembo Vivian!
Alikuwa mrembo sana kwa kweli,kwenye uumbaji wake basi Mungu alitulia na kumpendelea sana Vivian!
Sura yake yenye asili ya kiarabu,umbo lake la kibantu na urefu wake vilinifanya nizame kwake mzima mzima!
Nikajitosa kwenye kuomba jimbo,bahati nasibu nikabahatika!Vivian akanikubali na tukaingia kwenye mahusiano!
Lakini ni Vivian huyu ndiyo amenifanya niichukie shule na nisiitamani tena!
Wakati huu mama ananiamsha kwenda shule,Mimi sikuwa naiwaza tena shule,nilikuwa nawaza maisha jinsi ya kupata pesa ili nimfurahishe mpenzi wangu Vivian!
Maneno yake jana yake yanilivunja moyo na kunifanya nijione kama kijana nisiyefaa!
Unajua ilikuwaje?tulikuwa na kawaida ya kukutana mahali fulani kupoza miili yetu pale ambapo tulihisi miili yetu inahitaji kugusana na kufanya lile tendo tamu kuliko yote!
Siku ile kama kawaida nilipokuwa shule nilimpenyezea ujumbe mpenzi wangu Vivian uliokuwa umeandikwa!
"TUKUTANE PALE PALE KWA SIKU ILE,NIMEKUMISS MPENZI WANGU!"
Ujumbe ulimfikia Vivian,nikamuona amenitupia jicho akatabasamu na kunikonyeza!
Nilifurahi sana nikaamini itakuwa Kama siku zote,tutafanya ngono na kufurahia maisha!
Baada ya kutoka shule tu nilirudi nyumbani nikabadili nguo zangu kisha nikatoka na kwenda tulipoahidiana na Vivian!
Ilikuwa sehemu fulani kuna kilima ambacho hakikaliwi sana na watu!
Nilifika wa kwanza Basi nikamsubiri mpenzi wangu Vivian ambaye alifika baada ya nusu saa!
Tofauti na siku zingine,Vivian hakuonyesha tabasamu usoni mwake,sikujua kwanini?na wala sikutaka kuuliza!
Nilijua atakuwa sawa tu na tutafanya ngono kama kawaida yetu kwenye eneo lile la mafichoni!
Nilimvuta na kumkumbatia kwa nguvu basi nikaanza kumpapasa huku na kule,lakini Vivian wangu ni kama mawazo yake hayakuwa pale!
Wakati naendelea kumpapasa alinisukuma kwa nguvu nikaangukia pembeni!
"Kenny,maisha haya mpaka lini?",aliniuliza nikashindwa kulielewa swali lake!
"Unamaanisha nini Vivian!"
"Hivi tutakutana huku kwenye vichaka mpaka lini?mi nimechoka kwa kweli,rafiki zangu wananisimulia wanapelekwa gesti nzuri na wapenzi wao,huku kwenye vichaka na majumba mabovu mi siwezi kwa kweli,nimechoka!"
Nilisimama nikiwa naelewa kwanini Vivian hayupo sawa,kumbe alitaka nimpeleke gesti,kumbe alichoka kila siku kukutana kwenye majani na k
utandika kanga yake chini!
Nilimsogelea kwa upole nikamshika mkono nikamuambia!
"Mpenzi wangu,lakini unajua fika Mimi ni mwanafunzi na siwezi pata pesa ya gesti!"
"Kenny mbona yule Idrisa ni mwanafunzi tena yupo kidato cha tatu na anampeleka Fahyma gesti nzuri tu!"
"Lakini mbona inajulikana yule anafanya biashara haramu shuleni,na hata akiwa mtaani huku anauza bangi!"
"Kenny wewe ni mwanaume,mwanaume wa kweli anampa mpenzi wake kitu anachokitaka!"
"Vivian vumilia nikimaliza shule nitatafuta kazi nzuri na hakika utafurahi!"
"Basi tusiwe wapenzi hadi tukimaliza shule!",alisema Vivian akataka kuondka nikamshika mkono!
"Vivian unaenda wapi mpenzi?"
"Naona haunielewi,mi naona tuachane tu mpaka tukimaliza shule tutarudiana!
"Hapana Vivian nakuahidi hatutakutana tena hapa,nitapambana kwa hali yoyote Ile ili nikupe unachotaka malikia wangu tafadhali usifikie maamuzi hayo!"
Hapo Vivian alisimama akaniangalia kwa dakika kadhaa kisha akaniuliza!
"Kwahiyo umesema Leo ni ya mwisho?"
"Ndiyo ya mwisho mpenzi wangu!"
"Ukinidanganya?"
"Siwezi kukudanganya,nakupenda Vivie!"
Basi hapo Vivian alitabasamu kisha akaifungua kanga yake akaitandika chini,akanirukia na kunipa ulimi wake tunaanza kudendeka!
JE NINI KITAENDELEA?USIKOSE KUFUATILIA MKASA HUU WA KWELI!
UNAWEZA KUPATA HADITHI HII HADI MWISHO KWA SH 5000/= TU
Lipia hapa 👉👉👉0716352102 AU 0744872552 (NAMBA ZOTE ZIPO WHATSAPP!
#LIKE #LIKE #LIKE
#COMMENT #COMMENT #COMMENT
#SHARE #SHARE #SHARE
#MTAG_RAFIKI_YAKO_MFURAHIE_UTAMU_WA_HADITHI_PAMOJAAAAAA
Simulizi ya kweli.......SARAFINA SEASON 3(Historia ya GAIDI KENNY)
Msimuliaji.................Kenny Jonas
Mwandishi................Jack Mambo
Whstp..0752761388/0744872552
Call............................0716352102
Umri...........................18+